Back to top

APPLE YASITISHA MRADI WA MAGARI YA UMEME

29 February 2024
Share

Imeelezwa kuwa Kampuni ya Apple imeachana na mpango wake wa siri, iliyouanzisha kwa zaidi ya miaka 10 wa kutengeneza magari ya umeme yasiyo na dereva.
.
Kulingana na vyombo vya habari, ikiwemo #Bloomberg ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kutoa taarifa hiyo, imesema kuwa timu iliyokuwa ikishughulika na mradi huo itapunguzwa na baadhi ya wafanyakazi wa timu hiyo watahamishiwa kwenye idara ya akili bandia (Artificial Intelligence).
.
Hata hivyo, Kampuni hiyo ina miradi mingine inayohusiana na magari, ikiwa ni pamoja na programu yake ya infotainment #CarPlay, ambayo Apple inasema imewekwa kwenye 80% ya magari mapya.
.
Taarifa za Kampuni ya Apple kutengeneza gari zilianza kusambaa mnamo mwaka 2014, baada ya kampuni hiyo kuajiri wahandisi wa magari na vipaji vingine kutoka kwenye kampuni za utengenezaji magari, ingawa hapakuwa na taarifa za moja kwa moja kwa umma kutoka kwa kampuni hiyo kuhusu mradi huo.
.
Baada ya uamuzi huo wa Apple, Bilionea Elon Musk ambaye ni mmiliki kampuni ya utengenezaji magari, #tesla, alichapisha emoji ya saluti na sigara kwenye mtandao wa X.Com (zamani Twitter), ujumbe ambao ulitafsiriwa kuwa amefurahishwa na uamuzi huo wa Apple.