Back to top

TBA yakabidhi mabweni matatu na madarasa mawili Shule ya Msingi Luhira

29 March 2018
Share

Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA ) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili ya Shule ya Msingi Luhira ya watoto wenye ulemavu wa kutoona iliyopo katika halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano na Manispaa ya Songea, Meneja wa TBA Mkoa wa Ruvuma , Bwna. EDWIN NUNDUMA amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa mabweni matatu na ukarabati wa madarasa mawili kwa gharama ya Shilingi zaidi ya Milioni 151.

Kwa mujibu wa Meneja huyo kila bweni lina uwezo wa kulaza wanafunzi kumi-na-wawili hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi 36.

Mkuu wa shule hiyo, Bibi. JOYCE KONGA amesema shule hiyo ina wanafunzi 48 wanaolazimika  kulala wawili wawili kwenye kitanda kimoja.

Ameishukuru Serikali kwa kuwajengea wanafunzi hao mabweni ya kisasa na kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu.