
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila Machi 8, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda amewahimiza wanawake katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, kuhakikisha wanaimarisha vikundi vyao vya ujasiriamali kwa lengo la kujiletea maendeleo ili kujikwamua na maisha.
Mhe.Pinda ametoa kauli hiyo Kata ya Mwampuli Halmashauri ya Mpwimbwe mkoani Katavi, na kubainisha kuwa Halmashauri ya Mpimbwe imeweka utaratibu wa kupeleka maafisa wake kwenye kila Kata ya Halmashauri hiyo lengo kupokea kero za wanawake na baadaye kuzitafutia ufumbuzi.


Mhe.Pinda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kavu amewata wanawake hao kuweka utaratibu ikiwemo kuwa na uongozi imara utakaowezesha vikundi kutunza fedha na kufanya biashara.
Amewataka maafisa kutoka Halmashauri ya Mpimbwe hasa wale wanaohusika na mikopo kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa vikundi vya wanawake ili vijielewe katika shughuli zinazokwenda kufanya.
