Back to top

ASHTAKIWA KWA KUWAFUNGA WATOTO WAYA.

06 March 2024
Share

Mwanaume (45) mmoja wa Australia Magharibi, ameshtakiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kuwafunga mikono watoto watatu, kwa kutumia waya (cable), baada ya kudai aliwakuta wakiogelea katika eneo (swimming pool) ambalo halina uangalizi.

Polisi walisema mwanaume huyo, alikuwa amewazuia watoto hao akiwemo msichana (6) na wavulana wawili wenye umri wa miaka saba na minane, baada ya kuwakuta wakiogelea kwenye eneo ambalo halina uangalizi.

Video iliyosambazwa mtandaoni, imewaonyesha watoto wawili, wakiwa wamefungwa mikono huku wakiwa wanalia.

Maafisa wakuu wa serikali wanasema "wameshtushwa" na picha hizo, na polisi wametoa wito wa jamii kuwa na utulivu wakati wakilifanyia kazi suala hilo.

Mamlaka ilisema mwanaume huyo aliwapigia simu Jumatatu kuripoti tukio hilo huko Broome, takriban kilomita 2,000 kaskazini mwa Perth, akiwaambia kwamba alikuwa amewapata watoto hao kwenye "dimbwi lisilo na mtu".

#BBC