
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amepigilia msumari kauli yake ya kupelekwa wanajeshi wa Ulaya nchini Ukraine, na amewahimiza washirika wa Ukraine kutokuwa waoga katika kuiunga mkono nchi hiyo inapopambana na uvamizi wa Urusi.
Rais huyo amesisitiza kauli yake ya kutatanisha aliyoitoa wiki iliyopita kuhusu haja ya nchi za magharibi kuwapeleka wanajeshi wao nchini Ukraine Kauli ambayo iliibua gumzo barani Ulaya.
Rais wa Ufaransa, amesema katika mkutano wa pamoja na mwenzake wa Jamuhuri ya Czech, kwamba nchi hizo zinaungana katika kuiunga mkono Ukraine, kwenye vita vyake na Urusi na kwamba ziko tayari kutafuta njia mpya, za kuwasaidia Waukraine ili waweze kushinda vita hivyo.
#DW
