Back to top

UJENZI DARAJA LA RUAHA MKUU WAFIKIA 86%

07 March 2024
Share

Msimamizi Mkuu wa Matengenezo ya Barabara na Madaraja TANROADS Mkoa wa Mororgoro Mhandisi.Patrick Rambika, amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa Mkoani Morogoro ikiwemo Ujenzi wa Barabara ya Mikumi - Kidatu – Ifakara (sehemu ya Kidatu – Ifakara, (km 66.9) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu ambao umefikia asilimia 86% za utekelezaji na tayari Mkandarasi amekamilisha km 55.67 za lami kati ya km 66.9 zinazotakiwa kwa mujibu wa Mkataba.  

Mhandisi Rambika ameeleza kuwa Ujenzi wa Barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 142) kwa kiwango cha lami (sehemu ya Rudewa – Kilosa km 24) kwa kutumia fedha za ndani; Mkandarasi amekamilisha ujenzi wa kilometa 22.05; barabara imekabidhiwa na inatumika, Mkandarasi amekamilisha pia madaraja matatu ya Kobe, Wailonga na Mazinyungu na kwasasa anaendelea na kazi ya km 0.75 ya maungio ya madaraja hayo.

Amebainisha kuwa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (Kizuka Army Camp), 11.6km – Mradi umesainiwa tarehe 7 Februari 2024, Mkandarasi Mzawa, M/s Kings Builders Ltd atatekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 20.54 kwa muda wa miezi 12.

AMeongeza kuwa mradi wa Ujenzi wa barabara ya Bigwa – Kisaki; sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78, Mkataba umesainiwa tarehe 5 Februari 2024, na Mkandarasi M/s China railways 15 Bureau Group Corporation ya China atatekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 132.016 kwa muda wa miezi 27.

Mhandisi Patrick Rambika ameeleza hayo mkoani humo kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya miundiombinu ya ujenzi wa barabara na madaraja.

Pia amesema Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Ifakara – Mbingu, km 62.5;- Mkataba ulishasainiwa Mkandarasi ameshakabidhiwa 'Site' na ameanza kazi ya kujenga kambi na kuleta mitambo ya ujenzi.