Back to top

SMZ yakataa kuwa dampo la vyakula na dawa zisizofaa.

29 March 2018
Share

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikisha wananchi kuwa Zanzibar  itafuata sheria na serikali haitokubali kuona Zanzibar ndio dampo la vyakula na dawa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Msimamo huo umetolewa na waziri wa afya wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed  katika hotuba yake iliyosomwa na naibu waziri wa afya Mhe. Harusi  katika uzinduzi wa    Zanzibar kujiunga kimataifa na mfumo wa TEHAMA  wa  ukaguzi na uingizaji wa vyakula na dawa nchini ambapo kupitia wakala wa vyakula na dawa Zanzibar inakuwa nchi ya tano  katika ukanda wa Afrika Mashariki   ambapo Mhe. Waziri amesema serikali   imepania kuona vyakula na dawa zinazoingia zimedhibitiwa na wakala na kusajiliwa ndani na nje.

Mapema  mkurengezi mtendaji wa wakala  wa vyakula na dawa Zanzibar Dkt. Burhan  Simai amesema kuanza kwa mfumo huo utaleta mabadiliko makubwa Zanzibar kwa jamii ikiwa ni pamoja kuhakikishiwa vyakula na dawa  zinatambulika na  huduma kupatikana  kwa muda mfupi,huku  mkurugenzi wa TRADEMARK East Africa  John Ulanga ambao ndio wafadhili na wasimamizi  wakuu wa mradi huo,amesema tasisi hiyo itaendelea kuona ushindani wa kibiashara wenye tija unaendelezwa.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wadau mbali mbali wa taassi za serikali za huduma za vyakula na dawa na pia wafanyabishara unaifanya Zanzibar kuungana kimatifa na Tanzania bara, Kenya ,Uganda na Rwanda.