
Mfanyakazi wa Google aliyejulikana kwa jina la Linwei Ding, almaarufu Leon Ding, mwenye umri wa miaka 38, raia wa China na Mkazi wa Califonia nchini Marekani, ameshtakiwa kwa kosa la kuiba siri muhimu za kibiashara, zinazohusiana na mradi wa Akili Mnemba (Artificial Intelligency), na kuzipeleka kwenye kampuni mbili za China zinazojishughulisha na miradi ya Akili Mnemba, alizokuwa akifanya nazo kazi kwa siri.
.
Ding ambaye aliajiriwa na Google mnamo mwaka 2019 kama Mhandisi wa Program, ameshtakiwa kwa makosa manne ya wizi wa siri za biashara, ambapo kila kosa moja lina adhabu ya hadi miaka 10 jela na faini ya Dola 250,000 sawa na Tsh. 637,500,000/=.
.
Kulingana na Mashtaka aliyosomewa Ding, imeelezwa kuwa Data alizoziiba hutumika katika vituo vya ngazi za juu vya Google, na kwamba hutumika katika kusaidia mashine za akili mnemba kujifunza.
