
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa nchi yake, inaliunga mkono kikamilifu kundi la wanamgambo la Hamas.
Rais Erdogan ameeleza hayo kwenye taarifa aliyoitoa mjini Instabul na kubainisha kuwa hakuna anayeweza kuwashawishi kuliorodhesha kundi la Hamas kama la kigaidi na kwamba Uturuki ni taifa linalowasiliana kwa njia za wazi na viongozi wa kundi hilo.
Erdogan ni mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israel tangu kuanza kwa vita katika ukanda huo wa Gaza, ambapo amekaririwa mara kadhaa akiukosoa utawala wa Israel na kuushutumu kwa kufanya kile amekiita mauaji ya kimbari kwenye Ukanda wa Gaza.
