Back to top

RAIS SAMIA ATEUA 9 NA KUHAMISHA WENGINE

12 March 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi tisa na kuhamisha wengine watatu.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Wakuu wa Wilaya za Lushoto na Pangani, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Makatibu Tawala.

Pia Rais Samia amefanya uhamisho kwa Wakurugenzi Watendaji watatu wa Halmashauri.