Back to top

MACRON AKABILIWA NA UKOSOAJI KWA WAPINZANI WA KISIASA

12 March 2024
Share

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, anakabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wahudumu wa matibabu, wapinzani wa kisiasa na Kanisa Katoliki kuhusiana na rasimu ya muswada wa sheria inayoruhusu kuwasaidia watu kufa.

Muswada huo unatarajiwa kujadiliwa bungeni mwezi Mei mwaka huu na kama utapitishwa, utaruhusu kusaidiwa kufa kwa baadhi ya wagonjwa walio katika hali mahututi.

Rais Macron ameyaambia magazeti kuwa muswada huo utajumuisha masharti makali kuhusu kuwaruhusu watu kujichoma wenyewe sumu au kumuomba mwanafamilia au mhudumu wa matibabu kama hawawezi kujifanyia hivyo.

Hatua hiyo inajiri baada ya bunge la Ufaransa wiki iliyopita kuweka katika katiba ya nchi haki ya kutoa mimba na kuwa ya kwanza ulimwenguni kufanya hivyo.

Taarifa ya pamoja waliyoitowa na mashirika ya wauguzi na watoa huduma kwa wagonjwa wa saratani wamesema wamefadhaishwa, kukasirishwa na kuhuzunishwa na mpango huo.