Back to top

23 WAFIKISHWA KIZIMBANI TUHUMA DAWA ZA KULEVYA.

13 March 2024
Share

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) wamewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Watu 23 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Washitakiwa wamefikishwa mbele ya Mahakama hiyo kujibu tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi, heroin na mirungi kinyume cha Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Sura 95 marejeo ya mwaka 2019 kifungu cha 15 A Kifungu kidogo (1) (2) na kifungu cha 17. 

Akisoma Mashauri hayo 18 ya Jinai leo tarehe 12 Machi, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Christina Chovenye, wakili wa Serikali John Hamenya alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti katika mwezi Februari na Machi mwaka 2023 katika wilaya ya Kahama huku wakijua wazi kuwa biashara hiyo ni kosa kisheria.

Hamenya amewataja watuhumiwa hao 23 ambao wamefikishwa mahakamani kuwa ni, Juma Lusangija (54), Mwajuma kavula(36), Tayson Mwita Marwa (23) Emmanuel Christopher (33), Amos Augustino 34, wakazi wa mtaa wa Mwime na Fred Bichuka(37) , Rojasi Daudi (18) wakazi wa mtaa wa Mhungula na Juma Merengo Merena (44) mkazi wa Kidete , Hassan ally Ngwenyau (27) mkazi wa Nyakato na Gerald Emmanuel (18) mkazi wa Nyasubi.

Wengine ni pamoja na Paulo Charles Wilson (25) Nyakato, Joseph Lugenzi, Zamoyoni Andrea (26) mkazi wa Nyashimbi , Kobelo Ntahondi(42) Mkazi wa Bukondamoyo, Raphael Masanja (37) mkazi Nyakato na Said Kayoka kayoka (27) mkazi wa Mhungula, Saidi mselem (22) mkazi wa Majengo, na Haitham salum Suleiman (31) mkazi wa Nyasubi.