
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda, amewataka wananchi wa Ruangwa mkoa wa Lindi kutobabaika pale mwekezaji anapotaka kununua ardhi wanayomiliki.
Mhe.Pinda amesema hayo katika Kijiji cha Namkatila wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua utekelezaji wa mradi wa upangaji mipango ya matumizi ya ardhi katika halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi.
Amesema,wananchi hao wamepewa hati za umuliki wa ardhi na mwekezaji yoyote atakayejitokeza kuhitaji ardhi wanayomiliki basi taratibu za kisheria lazima zifuatwe.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kupanga matumizi ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Ruangwa . Aidha, Kamati pia ilikabidhi vyeti vya ardhi ya vijiji, ramani za mipaka iliyopimwa na kuhuishwa, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na Hati za Hatimiliki za kimila kwa wanachi.
