Back to top

RAIS AMPA MAJUKUMU YA 'FIRST LADY' BINTI YAKE

14 March 2024
Share

Katika uamuzi wa kihistoria, Rais wa Pakistan Asif Zardari ameamua kumtambulisha rasmi binti yake Aseefa Bhutto (31) kama 'First Lady' wa nchi hiyo, hali ambayo imeibua mjadala mzito wa kihistoria katika taifa hilo.

Hadhi ya 'First Lady' huwa inakwenda kwa mke wa Rais wa nchi lakini Zardari alikua mjane baada ya mkewe na Waziri Mkuu wa zamani Benazir Bhutto kuuawa mwaka wa 2007. 

Zardari hakuoa tena na nafasi ya mke wa rais pia ilibaki wazi katika kipindi chake cha kwanza kama rais wa nchi hiyo kuanzia 2008 hadi 2013.

Zardari, 68, aliapishwa kama rais wa 14 wa nchi hiyo siku ya Jumapili (Machi 10,2024) na amekuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa mara mbili katika nafasi hiyo.

Wakati wa hafla yake ya kula kiapo katika Ikulu ya Rais mjini Islamabad, Zardari aliandamana na binti yake mdogo, Aseefa.