Back to top

SONKO NA BASSIROU DIOMAYE FAYE WAACHIWA HURU

15 March 2024
Share

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, ameachiliwa huru siku chache kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo uliopangwa kufanyika Machi 24.

Bwana Sonko na msaidizi wake Bassirou Diomaye Faye, walikuwa katika gereza la Cap Manuel na kulakiwa na maelefu ya watu.

Wakili wa Sonko Bamba Cisse, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba, mteja wake aliyekuwa anazuiliwa gerezani pamoja na mshirika wake mkubwa Bassirou Diomaye Faye wameachiliwa huru.

Faye tayari ameteuliwa kuwa mgombea wa upinzani baada ya Sonko kuzuiwa kuwania nafasi hiyo na haikujulikana mara moja namna hatua hiyo inavyoweza kuwa na athari kwenye uchaguzi huo.

Sonko aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2019 anachukuliwa kuwa tishio kubwa kwa chama cha Rais Macky Sall, ambaye hagombei tena baada ya maandamano makubwa ya upinzani ya kumpinga na yaliyodumu kwa miezi kadhaa.