
Waziri Mkuu wa Israel Bw.Benjamin Netanyahu, amepuuza uwezekano wa kupatikana kwa mapatano huko Gaza, baada ya Hamas kutoa kile ilichokiita maono ya kina kwa wapatanishi.
Ofisi ya Bw.Netanyahu imesema Hamas inashikilia madai ambayo hayatekelezeki.
Amesema Hamas inataka kukomeshwa kabisa kwa vita na Israel ijiondoe kikamilifu kutoka Gaza.
Wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas imesema watu ishirini waliuawa walipokuwa wakisubiri msaada.
Israel ilikanusha na kudai mauaji hayo yalifanywa na Wapalestina waliojihami kwa kuufyatulia risasi umati huo uliokuwa ukisuburi chakula cha msaada.
