Back to top

USAJILI WA ZAHANATI YA NSHAMBYA KUWA HOSPITALI YA WILAYA UKAMILIKE

19 March 2024
Share

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imesikitishwa na ucheleweshaji wa upandishwaji hadhi ya Zahanati ya Nshambya, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, kuwa Hospitali ya Wilaya.
.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Mabula alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo, ambapo ameielekeza Halmashauri hiyo,  kukamilisha taratibu za usajili ili kuipandisha hadhi Zahanati hiyo.
.
"Inasikitisha sana kuona Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba hakuna watu wenye uchungu wa fedha zinazotolewa na serikali ambapo majengo yamejengwa 6, lakini linalotumika ni jengo la wagonjwa wa nje tu suala hili halikubaliki, hakikisheni hospitali hii inapata usajili na itumike kama ilivyokusudiwa na Serikali, majengo yanatumika kwa matumizi yasiyokusudiwa...wanatoa huduma ngazi ya Zahanati wakati majengo yaliyopo ni ya Hospitali ya Wilaya," amesema Mhe.Mabula.
.
Aidha, amesema Kamati hiyo ina jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za serikali za mitaa nchini hivyo wanakagua fedha zote zinazotolewa na serikali ili kuhakikidha zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na thamani halisi ya fedha ionekane.