Back to top

WANAOLAZIMISHWA KUFANYA KAZI WAONGEZEKA DUNIANI

20 March 2024
Share

Shirika la Kimataifa la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO) limesema utafiti mpya umeonesha kuwa idadi ya watu wanaolazimishwa kufanya kazi kinyume na matakwa yao imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni na kufikia wastani ya watu milioni 27.6 kwa siku.

Kulingana na takwimu mpya, miongoni mwa watu hao, ni wale ambao wako katika utumwa mambo leo, wakiwemo watoto zaidi ya milioni 3.3 pamoja na milioni 22 wanaolazimishwa kuolewa.

Aidha, utafiti wa ripoti hiyo ya ILO iliyotangazwa Jumanne unaonesha kwamba, watu hao wanaofanyishwa kazi kwa lazima wamezalisha karibu dola billion 236 za faida haramu kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko kubwa la dola bilioni 64 tangu mwaka 2014.

Utafiti huo imesema ongezeko hilo pia linatokana na Wasafirishaji haramu wa binadamu na wahalifu waowatumia wafanyakazi kwa nguvu, kujipatia karibu dola 10,000 kutoka kwa kila muathirika.

Utafiti huo umegundua kwamba mtindo ulioenea zaidi wa kazi za lazima ni biashara haramu ya ngono.

Ingawa inawakilisha asilimia 27 ya waathirika wote wa kazi za kulazimishwa, lakini ukandamizaji wa kijinsia inaingiza asilimia 73 ya jumla ya faida haramu inayopatikana.