Back to top

CHANGALAWE AMSHINDA BIBANO KWA RSC

20 March 2024
Share

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi "Faru Weusi wa Ngorongoro" Yusuf Changalawe amemchakaza mpinzani wake Maxinillano Bibano kutoka Equatorial Guinea katika round ya kwanza ya mchezo kwa kwa Mwamuzi kusimamisha pambano yaani RSC (Referee stop the contest) baada ya mpinzani huyo kuelemewa na Makonde mazito kutoka kwa Changalawe. 

Changalawe alitumia Dk 1 tu kumchakaza mpinzani wake na kuibuka na ushindi katika hatua ya robo fainali Uzani wa Light Heavyweight 80kg. 

Changalawe amejihakikishia kushinda medali na itakua medali ya 3 kwa Tanzania zote zikitokea kwenye mchezo wa Ngumi katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana. 

Mabondia wengine waliofanya vizuri ni Musa Maregesi (Cruiserweight 86kg) na Ezra Paulo Mwanjwango (Lightweight 60kg) ambao wote wako katika hatua za nusu fainali.