
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kutuma timu ya watalaamu kufika Wilaya ya Mwanga na kuchunguza matumizi ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.
Makamu wa Rais amesema hayo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo na kuonesha kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo ikiwemo msimizi wa mradi huo (Mhandisi wa kilimo) kutokuwa na vigezo vya kusimamia ujenzi wa hospitali.
Amesema miundombinu ya hospitali hiyo hairidhishi ikiwemo milango kuwa na viwango vya chini zaidi.
Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kusimamia kikamilifu mradi huo na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.
