
Viongozi wa dini wameiomba serikali kuanza kutoa elimu ya uraia kwa wananchi badala ya kusubiri kutumia gharama kubwa kununua silaha na mabomu ya machozi kwa ajili ya kudhibiti vurugu kwenye chaguzi zijazo.
Ujumbe wa viongozi wa dini wakati wa ibaada ya kitaifa ya pasaka ambapo wakrito nchini wanaungana na wenzao duniani kote kuadhimisha kifo na ufufuo wa bwana yesu,mbali na kuhimiza amani pia umeiomba serikali kuanza kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wajue misingi ya demokrasia na kudumisha amani na utulivu wakati wa chaguzi zijazo badala ya kusubiri kutumia gharama kubwa kununua siala kwa ajili ya kulinda amani.
Kwa upande wake askofu wa Kanisa Katoliki,jimbo la Mbeya,mhashamu baba askofu evarist marcus chengula amewataka wakristo kuomba mungu ili wakati wa uchaguzi utakapowadia wapate viongozi wenye mwelekeo wa kuwasaidia kujiletea maendeleo.
Baadhi ya wachungaji na waumini wa madhehebu ya kikristo wamesema kuwa taasisi za dini na serikali zote zina lengo moja la kuwaletea wananchi maendeleo,hivyo wanaweza kukaa pamoja na kushikiana wananchi kutimiza malengo yao.