Chama cha walimu wa masomo ya Sayansi na hesabu shule za sekondari nchini wameeleza kuelemewa na wanafunzi kutokana na uchache wao uikilinganishwa na idadi ya wanafunzi.
Akizungumza na ITV Jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha sekretarieti Mwenyekiti wa chama hicho, Bwana DAMIANI EMMANUEL amesema nchi nzima wamejadili upungufu huo kufanya kushuka kwa masomo hayo pamoja na idadi ya wanafunzi wanapenda hesabu na sayansi kushuka mwaka hadi mwaka.
Amesema wameanza mchakato wa kushirikiana na wadau wa elimu kuanza kutumia maelfu ya walimu ambao wapo mtaani wakisubiri ajira kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Aidha upande wa walimu kutoka mikoa mbalimbali pamoja na kueleza mpango huo shirikishi kuwa na lengo la kuisaidia serikali katika kukabiliana na matatizo ya elimu.