Back to top

MWELI: WAFIKISHIENI MBOLEA WAKULIMA KWA WAKATI

01 May 2024
Share

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw.Gerald Mweli ameitaka Kampuni ya mbolea (TFC) kuongeza kasi ya kuwahudumia wakulima na kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati.

Mweli ametoa rai hiyo wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, maonesho yenye kali mbiu ya "From Lab to Farm".

Mweli pia amewashauri wadau wa kilimo kujikita zaidi katika uwajibikaji pamoja na kutumia zaidi teknolojia zinazotakiwa katika kuendeleza kilimo.

Akiwa katika Banda la wadau wa Ushirika, Katibu Mkuu Mweli alijionea namna mzani wa kidigitali unavyofanya kazi ikiwa pamoja na kupata maelezo kuhusiana na Benki ya Ushirika Kilimanjaro ( KCBL).