Back to top

NYONGEZA MISHAHARA MAMA, ATASEMA JAMBO HIVI KARIBUNI

01 May 2024
Share

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Mpango, amesema Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, amemuagiza awaambie wafanyakazi kuwa, kuhusu ongezeko la mshahara, wawe na matumaini kwamba atasema jambo hivi karibuni.
.
Dk.Mpango ameeleza hayo, alipomuwakilisha, Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Moi), ambayo Kitaifa imefanyika Jijini Arusha, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
.
"Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mama wa Taifa ameniagiza niwaambie wafanyakazi wa Tanzania, kuwa endapo hali hii itadumu, wafanyakazi wawe na matumani kwamba atasema jambo hivi karibuni, pamoja na hatua hiyo Serikali imeendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa namna nyingine mbalimbali, ikiwemo kwa kulipa nyongeza ya mwaka ya mshahara Annual Salary Increment" Mhe.Dkt.Philip Mpango