
Rais wa Zanzibar, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa wafanyakazi wa SMZ wataongezewa posho ya Tsh. 50,000/= ya nauli ili kuleta ufanisi katika kazi na kurahisisha masuala ya usafiri wakati wa kwenda kazini na kurudi nyumbani.
.
Mhe.Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Mei 01, 2024, katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) zilizofanyika uwanja wa Gombani, mkoani Kusini Pemba, ambapo amebainisha kuwa Tsh. Bil. 34/=, zimetengwa kwa ajili ya posho hizo.
.
Pia, Dk.Mwinyi amesema wamejipanga kutengeneza ajira 300,000 kulingana na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, huku akieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, kupitia shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ajira mpya zipatazo 187,651 zimepatikana.
