
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Pindi Chana, amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa maelekezo kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kampeni ya utoaji wa msaada wa kisheria ya 'Mama Samia Lagal Aid' inawafikia wananchi wa Mikoa yote nchini ambapo mpaka sasa tayari kampeni hiyo imefika katika mikoa 6 na hivi karibuni itafika Mkoani Njombe.
Waziri Pindi Chana amesema Rais Dkt.Samia ameiwezesha Wizara yake rasilimali watu pamoja na rasilimali fedha, ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na wananchi wengi wanapata msaada wa kisheria bila malipo yeyote.
