Back to top

WAZIRI MKUU WA SLOVAKIA APIGWA RISASI

15 May 2024
Share

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico, ameshambuliwa kwa risasi, akiwa mbele ya jengo la kituo cha kitamaduni ambalo lipo katikati mwa mji wa Handlova nchini humo, ambako alikuwa akishiriki katika mkutano wa Serikali.
.
Vyombo vya habari nchini humo, vimedai kuwa aliyefanya shambulizi hilo ni mzee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 71, na kwamba sababu ya kufanya tukio hilo bado halijafahamika.

Mtuhumiwa ambaye anadaiwa kumpiga risasi Waziri Mkuu wa Slovakia, akiwa chini ya ulinzi.


Kulingana na mtandao wa Reuters umedai kuwa shuhuda wake alisikia milio minne ya risasi wakati Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 59, alipokuwa akitoka nje ya jengo la kitamaduni, ili kusalimiana na umati wa watu, waliokuwa wakimsubili ili wasalimiane naye. #via #Reuters