
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetangaza kuwa kuna kimbunga katika Bahari ya Hindi, kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar ambapo imebainisha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla yakuanza kupungua nguvu.
.
TMA imesema kimbunga hicho chenye jina "IALY" hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini, kutokana na umbali kilipo kutoka kwenye nchi yetu, lakini vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.
.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imewashauri watumiaji wa bahari ya Hindi na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka kwenye Mamlaka hiyo pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

