
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limeteketeza hekari sita za shamba la bangi katika safu za milima Wota kwenye kijiji cha Mwanawota Wilayani Mpwapwa mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi Gilles Murroto amesema mbali ya kuteketeza hekari hizo wanawashikilia watu watatu kwa kuhusika na shamba hilo.
Naye mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw.Jabir Shekimweri amesema kuanzia sasa wataanza kuwaajibisha viongozi wa kata na vijiji ambao bangi zitakutwa katika maeneo yao.
Kuteketezwa kwa hekari hizo sita za bangi kunafanya idadi ya bangi zilizotetekezwa katika kipindi cha wiki moja wilayani humo kufikia tani kumi na nusu.