Back to top

RAIS WA IRAN EBRAHIM RAISI AFARIKI DUNIA

20 May 2024
Share

Makamu wa Rais wa Iran Mohsen Mansouri, amethibitisha kutokea kwa kifo cha Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi, ambaye amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea jana, Mei 19, 2024.
.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea karibu na Mji wa Jolfa ulio jirani na Taifa la Azerbaijan na kiasi umbali wa kilometa 600 kutoka Mji Mkuu wa Iran, Tehran, wakati Rais huyo alipokuwa safirini kutokea nchini Azerbaijan, alipokwenda kuzindua bwawa la kufua umeme.
.
Mabaki ya helikopta hiyo aina ya Bell 212 iliyotengenezwa Marekani, iliyokuwa imewabeba Rais huyo na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian yamepatikana mapema leo, Mei 20, 2024, baada ya kutafutwa usiku mzima tangu jana.
.
Kiongozi huyo amefariki akiwa umri wa miaka 63, na alichaguliwa kuwa Rais wa Iran mwaka wa 2021, na tangu aingie madarakani ameamuru kuimarishwa kwa sheria za maadili. #via #Reuters