
Serikali imesema hali ya mipaka ya nchi yetu iko salama na zinapotokea changamoto zinafanyiwa kazi.
.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Stergomena Tax, leo Mei 20, 2024, Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo ambapo ameeleza kuwa wanaendelea kuliwezesha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kwa zana, vifaa na mifumo ya kisasa ili liendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
.
Dk Tax ameliomba Bunge lipitishe bajeti ya wizara hiyo kiasi cha Shilingi Tril. 3.3/= kwa mwaka wa fedha 2024/25.
