Back to top

IRAN YATANGAZA SIKU TANO ZA MAOMBOLEZO KIFO CHA RAIS EBRAHIM

21 May 2024
Share

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ametangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo, Ebrahim Raisi, huku  Makamu wa Rais Mohammad Mokhber akiteuliwa kushika madaraka ya muda.

Vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimesema uchaguzi utafanyika tarehe 28 Juni ili kuchagua rais mpya.

Hata hivyo Baraza la mawaziri la Iran pia limemteua naibu waziri wa mambo ya nje Ali Bagheri Kani kuwa kaimu waziri wa mambo ya nje.

Wakati Iran ikitangaza siku Tano za Maombolezo, Rais Ebrahim Raisi amesfariki dunia katika ajali ya helikopta eneo la milima kaskazini-Magharibi mwa Iran, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian.