Back to top

BASI LA TAK BIIR LAPINDUKA, WATU KADHAA WAJERUHIWA

23 May 2024
Share

Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi la abiria aina ya Higer, mali ya kampuni ya TAK BIIR, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Katoro mkoani Geita kupinduka, katika eneo la Manga nje kidogo ya Manispaa ya Singida.
.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amon Kakwale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameeleza kuwa hakuna kifo hata kimoja kilichotokana na ajali hiyo lakini kuna majeruhi ambao idadi yao haijajulikana na wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mandewa kwa ajili ya matibabu.
.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, ingawa baadhi ya mashuhuda wameeleza kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akilikwepa gari dogo lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara.