Back to top

TAARIFA ZA WANANCHI ZILINDWE NA MATAPELI WA MIKOPO.

27 May 2024
Share

Serikali imeombwa kuongeza nguvu ya kudhibiti na kuimarisha mifumo ya Taasisi zinazohusika na utunzaji wa taarifa binafsi za wananchi, kuhakikisha zinalinda taarifa hizo ili kuepusha taarifa hizo kufikiwa na watoa huduma ya mikopo wasio waadilifu ambao hutumia taarifa hizo kuwapigia simu wananchi na kuwashawishi watu kukopa.

Rai hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Baraka Mafwimbo, kupitia Kampeni Maalum ya kutoa elimu ya masuala ya fedha yaliyolotewa na wizara ya fedha  kwa Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Missenyi SP. Jonas Sira Soa.

 “Binafsi nimewahi kupigiwa simu na kushawishiwa kuchukua mkopo na watoa huduma ambao sikujua taarifa zangu wamezitoa wapi, lakini walikuwa wananielezea kama wananifahamu lakini hawakuweza kufanikiwa kwa kuwa nimewahi kupata elimu ya masuala ya fedha zamani’. Mkaguzi wa Polisi Baraka Mafwimbo.


 
Kwa upande wake Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, aliwasisitiza wananchi na polisi kuhakikisha wanatumia kuomba mikopo kwenye Taasisi za Fedha zilizosajiliwa rasmi ili kujiepusha na matapeli.
  
Alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha, itaendelea kutoa elimu ya masuala fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha ikiwemo elimu ya mikataba, uwekezaji na mikopo umiza.