Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakta. FAUSTINE NDUGULILE amesema azma ya Serikali ya kuhakikisha kila wilaya nchini inakuwa na hospitali ya kisasa ya wilaya ipo palepale.
Dakta. NDUGULILE ameliambia Bunge kuwa azma hiyo ina kwenda pamoja na Serikali kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga hospitali za wilaya katika wilaya ambazo hazina hospitali zenye hadhi inayotakiwa.
Amesema mbali ya hilo Serikali itahakikisha kuwa hospitali hizo zinakuwa na watumishi wa afya na dawa za kutosha kama inavyotakiwa.
Naibu Waziri NDUGULILE alikuwa akijibu maswali ya wabunge ambayo yalielekezwa kwa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, Wazee na Watoto.