
Wizara ya Ujenzi imeanza utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia (PPP), katika kutekeleza miradi ya miundombinu.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Mh.Innocent Bashungwa, wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024.
Amesema lengo ni kutumia utaratibu huo ni kuipunguzia Serikali gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya miundombinu hasa barabara na madaraja, ambayo Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha.
Aliitaja miradi inayotekelezwa kwa utaratibu huo kuwa ni ujenzi wa barabara ya Kibaha-Chalinze-Morogoro-Dodoma (Expressway), yenye urefu wa kilometa 423.8 kwa mfumo wa kulipia.
