
Katika kuiimarisha timu ya Simba SC, imetajwa kuwa hivi karibuni itakamilisha usajili wa Nahodha wa timu ya Vipers ya nchini Uganda, Milton Karisa, kwa kandarasi ya miaka miwili.
.
Imeelezwa kuwa Karisa anauwezo wa kucheza nafasi tatu za juu kama winga wa kulia, kushoto na kati na nafasi anayoihudumu zaidi ni kushambulia kutokea kulia na anatumia mguu wa kulia.
.
Nahodha huyo ambaye mpaka sasa klabu yake ya Viper, inatambua kuwa ataondoka kwa sababu mkataba wake umefika ukingoni na hajaonesha nia ya kusalia kwenye klabu hiyo, katika msimu huu ameifungia timu hiyo mabao 9 pamoja na assist 5.
.
Aidha, Mchezaji huyo ameeleza kuwa Simba ni klabu kubwa hata yeye anashauku ya kuona mchakato huo unakamilika, ambapo amesisitiza kuwa hatowaangusha wakifanikiwa kupata saini yake.
