
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman, ameshuhudia utiaji saini mkataba wa mashirikiano (MoU), baina ya Taasisi mbili za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), katika nyanja mbalimbali za utekelezaji wa majukumu yao.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma na Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF, Nassor Shaaban Ameir.
Hafla hiyo imefanyika mjini Unguja, pamoja na ufunguzi wa kikao kazi baina ya WCF na Divisheni za Mahakama Kuu pamoja na Mahakama Kuu ya Zanzibar, kujadili sheria za haki za kazi.
Halfa hiyo pia imeshuhudiwa na Jaji Kiongozi, Mhe. Mustafa Siani, ambaye alimuwakilisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga, Majaji wa Mahakama Kuu na Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
