Back to top

Serikali kuwadhibiti Mawakala wanaowatafutia kazi Watanzania ughaibuni

06 April 2018
Share

Serikali imesema itaendelea kuwadhibiti mawakala wanaoshughulika na kuwatafutia Watanzania ajira nje ya nchi ili kuwafanya waajiriwa hao wawe salama.

Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Masharika Dkt.Suzan Kolimba amesema hayo Bungeni wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake kuhusiana na Watanzania walioajiriwa nje ya nchi.

Amesema Watanzania wanatakiwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na nchi katika kusimamia suala la ajira nje ya nchi la sivyo watakuwa wakijiweka katika njia panda.

Katika maswali hayo Serikali iliulizwa jinsi inavyopambana na matatizo ambayo Watanzania wanayapata wanapoajiriwa nje ya nchi ikiwemo kunyang'anywa simu huko wanapoajiriwa.