Back to top

'WIZARA YA NISHATI ONGEZENI KASI USIMAMIZI WA MIRADI'

07 August 2024
Share

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Nishati kuongeza nguvu katika kusimamia miradi yote ya nishati, ili ikamilike kwa wakati na kuwawezesha wananchi kupata nishati ya uhakika.

Rais Samia ametoa agizo hilo mkoani Morogoro.

"Nimejionea mwenyewe wakati naenda Kilosa tofauti iliyokuwa ikionekana maeneo ambayo hayana umeme na yale yenye umeme ambayo yameshamiri kwa shughuli za biashara, hii inaonesha umuhimu wa nishati katika maeneo yote nchini." Amesisitiza Dkt.Samia

Aidha, Rais Samia ameutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha mapema kupeleka umeme kwenye Vijiji vilivyobaki na kuongeza kasi ya kusambaza umeme kwenye Vitongoji ili wananchi waweze kufanya kazi za maendeleo.