Back to top

RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO WA 44 WA SADC

15 August 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, anaondoka leo kwenda Harare, Zimbabwe, kuhudhuria Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC utakaofanyika tarehe 17, Agosti 2024.

Taarifa ya Ikulu imesema Katika mkutano huo, Rais Dakta Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,akipokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema anayemaliza muda wake.

Kauli mbinu ya mkutano huo ni Kukuza Ubunifu ili Kufungua fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kuelekea SADC yenye viwanda.