Back to top

DODOMA NA MIKAKATI YA KUPAISHA USHIRIKA

16 August 2024
Share

Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Dodoma wamepewa wito wa kutimiza majukumu kwa kufuata Kanuni Taratibu na Sheria za Ushirika ili kuviwezesha Vyama kuongeza tija na manufaa kwa Wanachama.

Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Joseph Chitinka amebainisha hayo akifungua Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Wajumbe wa Bodi, Kamati za Usimamizi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika mkoani Dodoma. 

Mafunzo hayo yamejikita katika kuwajengea uwezo Vyama vya Ushirika katika masuala muhimu ya kuzingatia kwenye uandaaji wa Mikutano mikuu ya Vyama, uandaaji wa makisio ya Mapato na Matumizi pamoja na matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU).

Miongoni mwa masuala aliyosisitiza Mrajis Msaidizi ni pamoja na kuboresha na kujenga mahusiano bora ya kazi ili kuondokana na Migogoro mbalimbali, ubunifu katika utekelezaji wa majukumu, Vyama kuhakikisha vinaondokana na Hati Chafu, kujua mahitaji sahihi ya mafunzo kwa Watendaji, Vyama kujiendesha kibiashara pamoja na kuunda Majukwaa ya Wanawake, Vijana na Wazee.