
Mamlaka ya Maji mji wa Kisarawe ina upungufu wa maji, Lita za ujazo zaidi ya Elfu moja ili kukidhi mahitaji ya wateja wake wapatao kaya 468.
Meneja wa mamlaka hiyo Wilayani Kisarawe, Bwana. THURWAY NINGA amesema kwa sasa wanazalisha Lita za ujazo 540 wakati mahitaji halisi yanayotosheleza ni Lita za ujazo 1,578.
Ameonegza kuwa kutokana na hali hiyo kutoa huduma kwa wateja wapya ambao ni sawa na ongezeko la asilimia ishirini walioomba kuungansihiwa huduma ya maji mjini humo inakuwa vigumu.
Hata hivyo Bwana.NINGA amesema mradi mkubwa wa maji kutoka Ruvu ambao unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu, utawezesha kuwahudumia wateja wapya ambao pamoja na kutuma maombi wanasubiri.