Back to top

Rais Dkt. Magufuli azindua nyumba za makazi ya askari Polisi Arusha.

07 April 2018
Share
Gwaride la heshima kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likipita mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018

Rais Dakta. JOHN POMBE MAGUFULI amesema Serikali itaendelea kuliimarisha Jeshi la Polisi kwa kuboresha Miundombinu, vitendakazi na Maslahi ya askari na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo wakati wote.

Rais amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP SIMON SIRRO kuhakikisha askari wanatumia mbinu za kisasa kukabiliana na  kilimo cha bangi na kuacha mara moja kwenda kufyeka na kuchoma mashamba ya bangi.

Ameyasema hayo katika uwanja wa Sheikh Amry Abedi Jijini Arusha alipokuwa anazungumza na maelefu ya wananchi baada ya  kuzindua nyumba 31 za makazi ya polisi, kituo cha utalii na kushudia mazoezi ya askari polisi ya kukabiliana na uhalifu.

Rais Magufuli ambaye ametoa Shilingi BILIONI kumi kwa ajili ya kuboresha Makazi ya Polisi kote nchini amewapongeza  viongozi wa Mkoa wa Arusha kwa kuwashirikisha wananchi wakiwemo wawekezaji kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP SIMON SIRRO na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa MWIGULU NCHEMBA pamoja na  kumweleza Rais baadhi ya matatizo wamesema wanaendelea kuzikabili kwa kuimarisha vikosi vya doria usiku na mchana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018
Gwaride la heshima kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likipita mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Simon Sirro katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018

 

IGP Simon Sirro akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Masauni akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwiguli Nchemba akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akikaribisha wageni na kusoma risala ya mkoa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kikipita na kutoa heshiama jukwaa kuu baada ya kuonesha kazi zake katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018