
Makamu wa rais wa Mhe. Samia Suluhu Hassani amesema ipo haja ya jamii kuitumia mitandao ya kijamii katika kuhamasisha maendeleo na kuimarisha amani nchini badala ya kuwa chanzo cha kudumaza maendeleo na kuharibu hali ya utulivu na ambayo imekuwa nchini
Makamu wa rais amesema hayo katiks hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kwenye uzinduzi wa taasisi ya amani mkoani Dodoma na kuongeza kuwa serikali itatumia uwezo wake kuhakikisha mitandao ya kijamii inatumika vizuri.
Naye kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw. Simon Odunga amesema mkoa wa Dodoma upo shwari na kuwa serikali ngazi ya mkoa daima imekuwa mstari wa mbele kuufanya mkoa huo unaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine katika nyanja zote.