Back to top

DKT.KIJAJI AIAGIZA NARCO KUONGEZA UZALISHAJI MBEGU ZA MIFUGO

17 December 2024
Share

Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO, iliyopo Kongwa Jijini Dodoma Kuongeza wigo wa Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mifugo na Malisho itakayoongeza upatikanaji wa Nyama nchini na Kukuza uchumi wa Wafugaji.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo leo Wakati wa Ziara yake kwenye Kambuni ya Ranchi za Taifa NARCO na kuahidi kurudi Januari 5, 2025 ili kuona utekelezaji wa maagizo hayo.

Kuhusu uzalishaji wa Mbegu za Malisho Dkt Kijaji amemwagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya  Masoko Stephen Michael  kushirikiana na NARCO kukamilisha malipo ya Mkandarasi wa mradi wa visima sita wenye thamani ya milioni 700 ili visima hivyo vianze kutumika kuzalishia malisho.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO Aziz Mrima  amesema bodi hiyo inajukumu la kuifanya kampuni hiyo kuzalisha  mbegu bora za mifugo zitakazoweza kushindana na wafugaji wengine barani afrika hivyo ameahidi kuyatekeleza  maelekezo ya Waziri Dkt. Kijaji.

Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Stephen Michael  katika kutekeleza maelekezo hayo idara yake itaendelea kufuatilia ili kukamilika mradi huo ambapo hadi sasa tayari Bilioni 3.2 zimepatikana kwaajili ya Malipo hayo.