
Spika wa Bunge Mheshimiwa JOB NDUGAI ametoa ufafanuzi kuhusu watumishi wanne wa kambi ya upinzani Bungeni kuondolewa na kusema wamefanya uamuzi huo kwa kuzingatia masuala ya usalama.
Amesema watumishi wa kambi rasmi ya upinzani wapatao wanne walikuwa na mikataba ya muda mfupi sawa na watumishi wa kambi ya Chama Tawala waliokuwa watano ambao mikataba yao imeisha Desemba mwaka jana na kusema wote wameondolewa kufanya kazi hizo za Bunge.
Amewataka wabunge wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni kuchapa hotuba zao na kusisitiza kuwa uamuzo huo unakuja kutokana kile alichokitaja kuwa ni suala la usalama na jengo.
Kuhusu Mwenyekiti wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa FREEMAN MBOWE kutokuwa na gari amesema gari sio tatizo ilikuwa ni dereva ambaye amestaafu na muda wowote suala hilo litamalizika kwa sababu madereva wapo.
Spika amelazimika kutoa maelezo hayo ikiwa ni kujibu muongozo uliotolewa tarehe 12 mwezi huu na Mbunge wa Ukonga, Mheshimiwa MWITTA WAITARA aliyehoji kutokuwepo kwa wafanyakazi wanne wa kambi ya upinzani Bungeni.