Back to top

Shughuli za utalii katika ziwa Manyara zaanza tena baada ya kusimama.

18 April 2018
Share

Shughuli za utalii katika hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara zilizokuwa zimesimama kwa muda baada ya miundombinu ya barabara kuathiriwa na mvua sasa zimenaendelea baada ya maeneo yaliyokuwa yameharibiwa na  mafuriko kutengenezwa.
 
Meneja mahusiano wa shirika la hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) Bw.Pascal Shelutete amesema pamoja na  hatua hiyo shirika limechukua tahadhari katika hifadhi zote 16 ya kukabiliana na athari za mvua na kuhakikisha kuwa shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida na kwamba shirika litahakikihsa wageni wote  wanaendelea na safari zao kama kawaida.
 
Hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara ni miongoni mwa zilizokuwa zimeathiriwa na mvua zinazoendelea ambazo licha  ya kuzoa daraja muhimu katika barabara inayoingia katika hifadhi hiyo ziliharibu mioundombinu katika maeneo  mbalimbali ya hifadhi hiyo na pia hifadhi zingine.
.............