Back to top

Serikali yatoa ufafanuzi sababu za kukatika katika kwa umeme nchini.

18 April 2018
Share

Serikali imetoa ufafanuzi wa changamoto ya kukatika katika kwa umeme nchini ambayo imekuwa ikijitokeza huku ikidai kuwa ni kutokana na uchakavu wa miundo mbinu iliyojengwa zamani, na imetoa mda wa miezi miwili kuhakikisha suluhisho linapatikana kwa lengo la kuwezesha huduma mbali mbali za kijamii.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wilayani Urambo mkoani Tabora mara baada ya kuzindua uwashaji umeme wa REA awamu ya tatu katika kijiji cha jionee mwenyewe wilayani humo ambapo amesema, wakati serikali ikiendelea na kuongeza Megawati za umeme sambamba na kuzifanyia ukarabati njia za umeme. 

Aidha akijibu hoja za kutokuwepo na umeme wa uhakika katika wilaya za Urambo na Kaliua ambao haumwezeshi mwananchi kuendesha shughuli za kijamii, Waziri Kalemani amesema serikali inajenga kituo cha kupozea umeme katikati ya wilaya hizo ili kuondoa changamoto hiyo.
 
Wakitoa malalamiko yao kwa Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani, viongozi na wananchi wa wilaya ya Urambo wamesema shughuli zinazotegemea Nishati ya umeme hazifanyiki ipasavyo kutokana na umeme usio na uhakika, na hivyo kusababisha maendeleo kurudi nyuma.