
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema kuwa hali usalama nchini bado iko imara na kwamba Jeshi la Polisi Nchini limejipanga kuhakikisha linachukua hatua za haraka na za kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kuharibu Amani ya nchi ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
IGP Sirro, amesema hayo akiwa mkoani Dodoma wakati akikagua mafunzo ya utayari kwa askari wa vikosi mbalimbali vya Jeshi hilo.
Pia IGP Sirro amesema kuwa, kwa sasa matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto ya mepungua kwa kiasi kikubwa na kwamba yapo baadhi ya matukio kama mauaji yanayotokana na ulevi wa pombe na kujichukulia sheria mkononi.